Ukoo wa
Abahinda ambao ndio
unatokana na Omukama
Rumanyika aliyeitawala Karagwe wamefanikiwa kumpata
msemaji wao mkuu
wa Ukoo baada
ya mchakato wa
muda mrefu wa
kupata atakayeongoza vikundi
vya ukoo huo
ambao umesambaa maeneo
ya wilaya ya
Karagwe na Kyerwa
na kwingineko.
Mkutano wa
uchaguzi wa kumpata
kiongozi huyo ambaye
ni mwenyekiti wa
ukoo ulifanyika jana
Februari 27 mwaka
huu katika makao
makuu ya Omukama
Rumanyika maarufu kama
Omuchikari kilichopo Bweranyange
wilayani Karagwe na aliyechaguliwa kuwa
msemaji wa ukoo
ni GODSONI Gipsoni
William Rumanyika.
Katika uchaguzi huo
Godsoni Gipsoni Rumanyika
alishindana na wagombea
wengine nne
na yeye kuibuka mshindi huku
mwalimu Samueli Rwehindi
Rwabujeje akichaguliwa kuwa
katibu wa kamati
ya ukoo huo
baada ya kushika
nafasi ya pili
kwa kupata kura 18
za wanaukoo huo.
Mbali na
uchaguzi wa mwenyekiti
wa ukoo pia
ilichaguliwa kamati tendaji
ya ABAHINDA yenye
jumla ya watu
tisa lengo ni
kuhakiksha historia iliyoachwa
na Omukama Rumanyika
inalindwa ikiwa ni
pamoja na kutunza
makumbusho yake na
eneo zima la
utamaduni.
Kwa upande
wa viongozi wa
serikali waliohudhuria
mkutano huo wakatoa
wito kwa ukoo
huo kwa ajili
ya kulinda,kuendeleza na
kuhakikisha historia ya
watu wa Karagwe
ambao ni wanyambo
inasimama na isipotee
kwenye vitabu vya
kumbukumbu.
Afisa Utamaduni
wilaya ya Karagwe Aloyce Mjungu
ambaye pia alimwakilisha mkurugenzi
mtendaji wa wilaya
ya Karagwe akatoa
maelekezo na ushauri
wa nini kifanyike
kuhakikisha maeneo ya
kihistoria karagwe yanalindwa
na kuhifadhiwa vizuri.
Viongozi waliochaguliwa mwenyekiti
na Katibu wa
Abahinda wametoa neno
lao la shukrani
huku mwenyekiti aliyechaguliwa akitoa
ahadi ya kusafisha makao
makuu ya Omukama
Rumanyika na kuhakikisha historia
inalindwa kikubwa akaomba
ushirikiano.
No comments :
Post a Comment