Thursday, 18 February 2016

BARAZA LA MITIHANI TANZANIA NECTA LIMETANGAZA MATOKEO HUKU UFAULU UKISHUKA 1.85%




Baraza la  mitihani  Tanzania Necta limetangaza  matokeo ya kidato cha nne yaliyopangwa kwa mfumo wa division. ufaulu umeshuka kwa 1.85% MWAKA 2014 ufaulu ulikwa kwa mfumo wa  GPA  na ufaulu ulikuwa  69.76% na sasa ufaulu wa mwaka  2015  ni  daraja  (Divisioni)  67.91%


Waliofaulu daraja la kwanza ni asilimia 2.77, la pili ni asilimia 9.01 na tatu ni 13.56 huku daraja la nne wakiwa 42.57
Nafasi tatu  za  kwanza  kwa  wanafunzi  waliofanya  vizuri  zimechukuliwa  na  wasichana.

Shule zilizofanya  vizuri  kitaifa  ni  Kazirege ya Mkoani –Kagera, Alliance Girls-Mwanza, St Francis Girls-Mbeya, Alliance, Boys-Mwanza, Canossa-DSM, Marian Boys-Pwani, Alliance Army Rock-Mwanza, Feza Girls-DSM, Feza Boys-DSmM na Uru Seminary-Kilimanjaro

Baraza  limesema  waliofaulu  ni  robo  ya  watahiniwa  wote  huku watahiniwa  87 walifanya  udanganyifu  wamefutiwa  matokeo  yao.


No comments :

Post a Comment